Resumen del episodio
Licha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo. Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.
Licha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo. Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.
Episodios
Wanaharakati wa mazingira walalamikia athari za kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Lamu
EscuchadoLicha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo. Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.
Je unafahamu umuhimu wa kuzuia upotevu na uharibifu wa chakula?
EscuchadoMwaka huu ni maadhimisho ya saba ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu utupaji na upotevu wa chakula, ambao unachangia kati ya asilimia 8–10 ya utoaji wa gesi joto Lengo la maendeleo endelevu nambari 12.3 linalenga kuona dunia ikipunguza upot’evu na uharibufuwa chakula kwa nusu ifikapo mwaka 2030.
Septemba 22, siku ya kimataifa ya kutotumia magari mijini
EscuchadoWananchi katika miji mbalimbali ya dunia wanahimizwa kuacha magari yao binafsi nyumbani na kukumbatia mbinu zingine za usafiri zilizo endelevu kama kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu. Makala haya yanaangazia namna baiskeli za umeme zinaweza kuwa moja ya suluhu ya uchafuzi wa hewa kwenye miji unaotokana na sekta ya usafiri.
Kenya: Wanaharakati watoa mapendekezo mapya dhidi ya plastiki zinazochafua mazingira
EscuchadoKenya inakabiliwa na changamoto ya plastiki zinazotumiwa mara moja tu kama vile mifuko inayotumiwa sokoni kupakia mboga ambazo huchangia katika uchafuzi wa mazingira licha ya kupigwa marufuku. Ni Kutokana na hili ambapo wanaharakati wa mazingira wamekuja na mapendekezo mapya ya kukabiliana na tatizo hili, mbali na suluhu la uchakataji. Moja ya matokeo ya mapendekezo haya ni kuiweka Kenya katika nafasi ya uongozi wa kikanda katika uvumbuzi wa mifumo ya kutumia tena bidhaa. Hellen Kahaso Dena kutoka shirika la Greenpeace Africa amechambua swala hilo. Sikiliza zaidi kwa kubofya.
Kenya: Nyenzo(Tool) mpya inavyoanika matumizi ya ufadhili wa tabianchi Kenya
EscuchadoMatumizi ya ufadhili wa hali ya hewa imekuwa swala kuu kwa wadau wa mazingira, kutokana na mianya ya ufuatiliaji. Nchini Kenya, shirika la Transparency International, sasa linajaribu kuziba mwanya uliopo ambapowakenya watakuwa wakifuatilia miradi na matumizi ya fedha hizi nchini humo kupitia jukwaa jipya la mtandaoni la Climate Finance Watch Tool.