Afrika Ya Mashariki

Afrika Ya Mashariki

Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
00:00
00:00

Resumen del episodio

Wiki hii tumeangazia namna nishati safi na umeme wa uhakika inavyoibadilisha Afrika. Afrika Mashariki imeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta ya nishati. Tanzania imeongeza uwezo wake wa uzalishaji wa umeme kufikia takribani megawati 4,600 baada ya kuanza kwa uzalishaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere wenye uwezo wa MW 2,115. Kwa upande mwingine Ethiopia imeendelea kuongoza ukanda kupitia mradi wa GERD wenye uwezo wa MW 5,150, huku Kenya ikiendelea kuwa kinara wa nishati ya jotoardhi na Uganda ikiendelea kuimarisha uzalishaji kupitia miradi mikubwa ya umeme wa maji.

Episodios

167-

Afrika Mashariki: Nishati Safi na Mustakabali wa Afrika Mashariki

Wiki hii tumeangazia namna nishati safi na umeme wa uhakika inavyoibadilisha Afrika. Afrika Mashariki imeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta ya nishati. Tanzania imeongeza uwezo wake wa uzalishaji wa umeme kufikia takribani megawati 4,600 baada ya kuanza kwa uzalishaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere wenye uwezo wa MW 2,115. Kwa upande mwingine Ethiopia imeendelea kuongoza ukanda kupitia mradi wa GERD wenye uwezo wa MW 5,150, huku Kenya ikiendelea kuwa kinara wa nishati ya jotoardhi na Uganda ikiendelea kuimarisha uzalishaji kupitia miradi mikubwa ya umeme wa maji.

10 oct. 2026
166-

Kenya: Nafasi ya vijana kwenye siasa za Kenya kuelekea uchaguzi mkuu 2027

Tunaangazia siasa za Kenya na nafasi ya vijana katika hatua za awali za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Je, vijana wanaingia kwenye uwanja wa siasa kama wapiga kura tu, au wanataka kuwa wabeba jahazi la maamuzi ya taifa?

03 oct. 2026
165-

Safari ya Sudan Kusini kuelekea uchaguzi wake mkuu wa kwanza

Baada ya kusubiri kwa zaidi ya miaka 15 tangu kupata uhuru mwaka 2011, Sudan Kusini imepanga kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa kitaifa tarehe 22 Desemba 2026. Je, uchaguzi huo utafungua ukurasa mpya wa demokrasia au utaibua mzozo mwingine wa kisiasa katika taifa hilo changa zaidi barani Afrika?

26 sep. 2026
164-

EAC: Kesi za kisiasa au utawala wa kisheria

Katika kipindi cha miaka ya karibuni, viongozi wa upinzani katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki wameendelea kujikuta mahakamani wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo uhaini. katika Makala ya Afrika Mashariki, tunaangazia mwenendo wa kesi zinazowakabili viongozi wa upinzani katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, je, ni ishara ya kuimarika kwa utawala wa sheria au kuna maswali yanayoendelea kuulizwa kuhusu ushindani wa kisiasa?

11 sep. 2026
163-

Kenya yaanza safari ya kutafuta dira mpya, ruwaza ya 2030 ikielekea kufika ukomo

Kenya imeanza safari ya kutafuta dira mpya ya maendeleo baada ya Ruwaza ya Taifa ya Maendeleo 2030 kuelekea kufikia ukomo wake. Safari hii inakuja wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, ikiwa na dira yake ya pamoja ya mwaka 2050, inayolenga kujenga ukanda wenye uchumi shindani, miundombinu iliyounganishwa, viwanda, biashara, ajira na maendeleo ya watu.

21 ago. 2026